Murder Was the Case

Murder Was the Case
Murder Was the Case Cover
Soundtrack ya Wasanii mbalimbali
Imetolewa October 15, 1994
Imerekodiwa 1993-1994
Aina West Coast Hip Hop, G-Funk, Rap
Urefu 68:30
Lebo Death Row/Interscope
Mtayarishaji Dr. Dre
Dat Nigga Daz
Sam Sneed
Soopafly
DJ Quik
Devante Swing


Makadirio ya kitaalamu
Tahakiki za ushindi
Chanzo Makadirio
Allmusic 4.5/5 stars[1]

Murder Was the Case ni jina la kutaja filamu na albamu ya kibwagizo kifupi cha mwaka wa 1994 ambacho kimechezwa na Snoop Doggy Dogg. Filamu hii yenye urefu wa dakika 18 iliongozwa na Dr. Dre na Fab Five Freddy ikiwa na wendo wa hadithi ya kifo cha Snoop Dogg na kufufuka kwake baada ya kuingia mkataba na Shetani. Jina la filamu linatokana na wimbo wa Snoop ambao upo katika albamu yake ya kwanza, Doggystyle, ambao ulitoka mapema kabla ya filamu hii. Albamu ilishika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200 mnamo Novemba 5, 1994 ikiwa na mauzo yapatayo 329,000 katika wiki yake ya kwanza na vilevile ilipata kutamba katika chati za albamu Top R&B/Hip-Hop.

Wiki iliyofuata ilikaa nafasi ya juu ikiwa imeuza nakala 197,000 na kupewa hadhi ya Dhahabu. Albamu ilitunukiwa hadhi ya platinum 2x ikiwa na mauzo ya nakala 2,030,000. Wimbo wa "What Would You Do" iliingizwa katika kibwagizo cha Natural Born Killers na kilipata kichaguliwa kwenye Grammy Award for Best Rap Performance by a Duo or Group katika sherehe za ugawaji wa tuzo hizo mnamo 1996. Albamu ilitolewa tena ikiwa na DVD ya ziada yenye video 3 mnamo 11 Julai, 2006.

Tupac Shakur alilipwa $200,000 na mmiliki wa Death Row Records Suge Knight kurekodi wimbo kwa ajili ya albamu hii. Wimbo ulirekodiwa, lakini haujatumika katika toleo halisi la kibwagizo. Udaku ulioenea kuhusu rekodi yenyewe ni kati ya "Pain" ambao baadaye ulikuja kutumika kwa ajili ya kibwagizo cha filamu ya Above The Rim, "High Til I Die Interscope Version", ambao baadaye ulitolea upya na kutumika kwa ajili ya albamu ya Sunset Park wakati 2Pac yupo katika studio ya Death Row Records, na Unreleased Version Of R U Still Down. R U Still Down ni sawa na toleo ambalo lilitolewa mnamo 1997 katika albamu ya 2Pac ya "R U Still Down". Hata hivyo, wimbo una biti tofauti, beti ya kwanza ambayo awali haikuwepo, kiitikio cha kike, na beti ya pili na tatu ambazo zimerekodiwa upya ambazo pia zinafanana kabisa na beti 1-2 ya kwenye toleo la albamu ya R U Still Down.

  1. Murder Was the Case katika Allmusic

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search